
KATIBA YA YOUTH AGAINST HIV/AIDS FOR SUSTAINABLE DEVELOPMENT
(JANUARI 02 ,2012)
YALIYOMO: IBARA
UTANGULIZI……………………………………………………………………1
DIRA YA SHIRIKA……………………………………………………………...2 DHAMIRA YA SHIRIKA………………………………………………………..3 UTAMBULISHO WA SHIRIKA ………………………………………………...4 HADHI YA SHIRIKA……………………………………………………………5
MALENGO YA SHIRIKA………………………………………………………...6
SHUGHURI ZA SHIRIKA………………………………………………………...7
UANACHAMA…………………………………………………………………….8
UTARATIBU WA KUJIUNGA NA SHIRIKA……………………………………9
MUUNDO WA SHIRIKA………………………………………………………..10
SIFA ZA KUWA KIONGOZI WA SHIRIKA……………………………………11
MATUMIZI YA FEDHA ZA SHIRIKA………………………………………….12
UFUNGUAJI WA AKAUNTI YA BENKI………………………………………..13
MAREKEBISHO YA KATIBA……………………………………………………14
MUUNDO WA UENDESHAJI WA MIKUTANO YA SHIRIKA………………...15
UCHAGUZI WA VIONGOZI WA SHIRIKA……………………………………...16
MICHANGO YA WANACHAMA…………………………………………………17
MAPATO YA SHIRIKA……………………………………………………………18
RATIBA YA KUENDESHA VIKAO……………………………………………….19
KUVUNJIKA KWA SHIRIKA………………………………………………………20
UPITISHAJI WA SHIRIKA………………………………………………………….21
IMETHIBITISHWA………………………………………………………………….22

- UTANGULIZI
Katiba ni taratibu na kanuni zilizouundwa na wanajamii fulani au kikundi cha watu chini ya makubaliano maalumu kwa lengo la kuwasaidia kuishi katika mfumo wenye manufaa kwao na hata jamii iwazungukayo. UKIMWI ni ukosefu wa kinga mwilini unaosababishwa na virusi viitwavyo Virusi Vya Vkimwi (VVU).Youth Against HIV/AIDS For Sustainable Development (YAHFSD) ni shirika lisilo fungamana na kikunndi chochote cha dini,chama cha siasa,kabila wala serikali, ni shirika la kupamabana na maambukizi ya ukimwi kwa vijana wa kike na kiume wenye lengo la kutokomeza na kupinga vikali maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi hasa kwa vijana wa kike na kiume.
2. DIRA YA SHIRIKA
Vijana bila ya maambukizi mapya ya vvu.pia vijana kuwa kama nyenzo kwa wadau kuimarisha mipango,utekerezaji na ufuatiliaji wa programu zao za kinga ambayo itapunguza kwa kiasi kikubwa maambukizi mapya kwa asilimia 25% ifikapo mwaka 2020.
3. DHAMIRA YA SHIRIKA
I. Dhamira ya shirika hili ni kuzidisha na kuongeza juhudi za kinga zidi yaVVU zilizo bora zaidi,zinazo tokana na ushahidi na zinazoweza kufikiwa na vijana wote ndani ya mwitikio shirikishi unaongozwa na taratibu za shirika na wadau ambao ni vijana.miongozo ifuatayo ni kiga dhidi ya vvu inayo faa imezingatiwa wakati wa uandaaji wa katiba ya shirika la yahfsd
a. Mafanikio ya vvu dhidi ya vvu yanategemea utawala bora katika kutekeleza hatua.
b. Wajibu wa uwajibikaji ni mujibu kwa kufikia hatua za kinga dhidi ya vvu zilizo bora zaidi zinawezakufikiwa na vijana wote.
c. Kinga dhidi ya maambukizi ya vvu inahitaji ushirikishaji wa jamii yote.
4. UTAMBULISHO WA SHIRIKA
A. JINA LA SHIRIKA: Youth Against HIV/AIDS For Sustainable Development (YAHFSD)
B. MAKAO MAKUU: Dodoma Tanzania.
C. ANUANI: ………………………….
D. BARUA PEPE: info.yahfsd@yahoo.com
E. WAVUTI/BLOGS:………………………….
F. Shirika litatumia lugha ya kiswahili na kiingereza katika shughuri zake za utendaji na kama nyenzo ya mawasiliano pia ikiwezekana shirika litatumia tafsiri ya lugha zingine kwa manufaa ya shirika na kwa kufuata katiba ya shirika.
G. Shirika litakuwa na nembo na mihuri inayoonyesha shughuri zinazo fanywa na shirika kwa mujibu wa katiba ya shirika.
5. HADHI YA SHIRIKA
a) Shirika litajitegemea na kuwa na uwezo kwa kushitaki au kushitakiwa kwa jina la shirika la YAHFSD.
b) YAHFSD itakuwa na uwezo wa kupokea fedha kutoka ndani na nje ya nchi,au zawadi,kukopa kwa mujibu wa sheria za nchi.
c) Shirika litakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi mfano kuajiri au kufukuza kwa manufaa ya shirika kutegemea malengo yaliyomo ndani ya katiba.
6. MALENGO YA SHIRIKA
(I).LENGO KUU
(a). kuongezeka na kukubalika kwa mienendo salama zaidi ya ngono na kupunguza
mienendo hatarishi kwa vijana.
(II). MALENGO
a. Kupunguza wapenzi wengi wa ngono kwa vijana.
b. Kupunguza uwiano wa vijana wanaojihusisha katika ngono kati ya marika yote.
c. Kupunguza hatari ya uambukizaji wa vvu kupitia ukahaba kwa vijana.
d. Kuongeza upatikanaji na matumizi ya kondomu mara kwa mara kwa vijana.
e. Kutoa elimu tohara ya hospitali kwa wanaume vijana.
7. SHUGHULI ZA SHIRIKA
1) Kutoa elimu ya kupima UKIMWI kwa hiari hususani kwa vijana.
2) Kufanya tafiti mbalimbali zikiwemo za kiuchumi,kisiasa, kijamii na kiutamaduni zenye kulenga kuwawezesha vijana.
3) Kutoa elimu ya ujasiliamali, rushwa, haki za msing za binadamu, elimu rika, utalii, nafasi ya mwanamke katika jamii, elimu ya mazingira na ajira binafsi.
4) Kuwahuisha vijana juu ya uzalendo kwa taifa lao.
8. UANACHAMA
(I). wanachama waanzilishi: wanachama waanzilishi ni wale tu wanao kidhi vigezo vifuatavyo;
a. Awe Mtanzania.
b. Jinsia zote mbili ya kike na kiume
c. Awe ameshiriki mchakato wa upitishaji wa katiba kabla ya siku ya udahiri
d. Awe amekwisha wasilisha taarifa zake zikiwemo barua ya maombi ya kujiunga na shirika,taarifa za mrithi wake na taarifa zake za taaluma na anuani kamili katika ofisi ya mkurugenzi wa shirika kabla ya shirika kusajiliwa.
e. Awe na umri kati ya miaka miaka 13 na kuendelea.
f. Kifungu 8 (I) d ,kama mwanachama hataw asilisha taarifa zake ambazo zilifaa kuwepo katika kumbukumbu ya ofisi ya msajiri wa vyama,wizara ya mambo ya ndani Tanzania kifungu hiki kitamuondoa.
g. Awe ametoa ada na michango iliyoidhinishwa na shirika
h. Asiwe na shitaka au tuhuma za kosa au makosa ya jinai.
i. Awe na akili timamu
(II).Wanachama wa heshima kutokana na nafasi yake ya kazi na jamii ;wanachama hawa ni lazima wakidhi vigezo vifuatavyo;
a. Kiongozi wa serikali,dini na dhehebu au jumuiya inayotambulika kiserikali
b. Mdhamini au wadhamini
c. Mtanzania au asiye Mtanzania
d. Umri kati ya miaka 18 na kuendelea
e. Jinsia zote ya kike na kiume
f. Awe hakabiliani au hashutumiwi na kosa lajinai
g. Awe na akili timamu
(III).wanachama wa kawaida; wanachama hawa wanahitaji kukidhi vigezo vifuatavo;
a. Uraia ni taifa lolote duniani
b. Umri usio pungua miaka 13 na kuendelea
c. Wa/mgeni mwalikwa aliye alikwa na shirika kwa mujibu na taratibu zinazo liogoza shirika kwa kufuata sheria na katiba ya nchi.
d. Awe na akili timamu
9. UTARATIBU WA KUJIUNGA NA SHIRIKA
I. Mwombaji atashauriwa kuisoma katiba na kuielewa
II. Mwombaji atawasilisha vielelezo vinavyo tambulisha uraia wake
III. Mwombaji atashauriwa kuandika barua ya kuomba kujiunga na shirika
IV. Mwombaji atajadiliwa na kupokelewa na kamati tendaji na orodha yake kupelekwa kwenye mkutano mkuu ili kupata ridhaa ya kusajiliwa kupitia kibali cha ofisi ya mkurugenzi wa shirika
(A).UKOMO WA MWANACHAMA
1. kushindwa kuhudhuria vikao zaidi ya mara tatu mfululizo bila sababu za kimsingi
2. kushindwa kutoa ada na michango iliyo idhinishwa na shirika
3. Aliye fukuzwa uanacha anaweza kuomba upya uanachama kwa muda wa mwaka mmoja toka aliposimamishwa uanachama
(B).UTOVU WA NIDHAMU
I. Shirika halita ruhusu mwanachama kupiga kura, kupigiwa kura, kuchagua au kuchaguliwa kwa nafasi yoyote ya chama kama atakuwa amesimamishwa au kufukuzwa uanachama au hajatimiza masharti ya kuwa mwanachama wa YAHFSD
II. Mwanachama aliye adhibiwa hatoruhusiwa kutumia jina la shirika laYAHFSD au kutangaza shirika kwa manufaa yake binafsi.
(C). HAKI YA MWANACHAMA
I. Kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wa chama kwa nafasi zile tu zitakazo tolewa na ofisi ya mkurugenzi wa YAHFSD
II. Kupata gawio ndani ya shirika kwa kufuata utaratibu
III. Kujulishwa jambo lolote kwa mujibu wa sheria zilizowekwa na shirika
IV. Kupiga kura na kupigiwa kura.
(D).WAJIBU WA MWANACHAMA.
I. Kutoa ada na michango yote iliyoidhinishwa na shirika
II. Kutekeleza malengo kwa madhumuni ya shirika
III. Kulinda siri za shirika
IV. Kulinda katiba ya shirika
V. Kuhudhuria vikao vya shirika.
10. MUUNDO WA SHIRIKA
| OFISI YA MKURUGENZI
|
| OFISI YA KATIBU MKUUU A.katibu mkuu B.naibu katibu mkuu |
| OFISI YA FEDHA NA UTAWALA A.Muhasibu B.Ofisa Mipango na Miradi. D.Ofisa rasilimali watu |
| OFISI YA KURUGENZI YA HABARI NA MAWASILIANO A.afisa habari na mawasiliano. |
| KAMATI TENDAJI (PROGRAMS) 1) Madawa ya kulevya 2) Rushwa 3) Haki za binadamu 4) Ushauri nasaha 5) Ujasilia mali 6) Utamaduni na michezo 7) Jinsia na elimu kwa watoto na vijana 8) Elimu ya malezi kwa wazazi. 9) Utalii 10) Elimu ya mazingira |
| IDARA YA UFUATILIAJI NA TATHMINI A.Mwenyekiti ufuatiliaji na tathmini. B. Mkaguzi wa ndani. |
11. SIFA ZA KUWA KIONGOZI WA SHIRIKA
I. Awe na elimu ya kuanzia kidato cha nne na kuendelea
II. Uamunifu na tabia nzuri
III. Umri miaka 18 na kuendelea
IV. Awe na bidii na kujituma
V. Asiwe mnyanyapaaji kwa wenzake
VI. Asiwe na tuhuma za makosa ya jinai
VII. Ajue ligha ya Kiswahili na kingereza kwa ufasaha
VIII. Awe na ujuzi wa uongozi angalau miaka miwili na kuendelea.
IX. Awe na akili timamu.
X. Awe ametimiza masharti ya uanachama.
12. MATUMIZI YA FEDHA ZA SHIRIKA
Fedha za shirika zitatumika kwa kufuata taratibu zilizo wekwa na shirika kwa mujibu wa miongozo ya fedha.
13. UFUNGUAJI WA AKAUNTI YA BENKI
Fedha zote za shirika zitahifadhiwa benki yoyote inayotambulika kisheria.hivyo basi shirika litakuwa na watia saini kama ifuatavyo
1. Mkurugenzi mkuu wa shirika(mwenyekiti).
2. Muhasibu wa shirika
3. Ofisa ufuatiliaji na tathmini
14. MAREKEBISHO YA KATIBA
Katiba hii itafanyiwa marekebisho wakati wowote pale itakapo hitajika kwa matakwa ya wanachama wenyewe iwapo itaidhinishwa na mkutano mkuu wa wanachama wote, mwenyekiti ataratibu shughuri hiyo.
15. MUUNDO WA UENDESHAJI WA MIKUTANO YA SHIRIKA
a) Mkutano mkuu wa wanachama wote (mara mbili kwa mwaka)
b) Mkutano wa kamati tendaji
c) Mkutano wa idara ya ufuatiliaji na tathmini
d) Mkutano wa dharula(muda/wakati wowote).
16. UCHAGUZI WA VIONGOZI WA SHIRIKA
I. Viongogozi watachaguliwa na wengine kuteuliwa na ofisi ya mkurugenzi wa shirika kwa mujibu wa sheria za shirika
II. Iwapo itatokea dharula yeyote kama kufariki kwa kiongozi,kaimu wake atakaimu nafasi hadi muda wa uchaguzi utakapo wadia.
17. MICHANGO YA WANACHAMA
I. Mwanachama atalipa ada na michango ya kiingilio pindi atakapo kubaliwa kuwa mwanachama
II. Mwanachama atalipa michango yote ya shirika iliyo idhinishwa na kupitishwa na mkutano wa wanachama
18. MAPATO YA SHIRIKA
a) Kiingilio cha wanachama
b) Fedha kutoka kwa wahisani au mashirika mbalimbali duniani
c) Misaada kutoka serikali kuu na serikali za mitaa
d) Watu binafsi na asasi za kiraia
19. RATIBA YA KUENDESHA VIKAO
(a). Mtano mkuu
Shirika litafanya mkutano mkuu wa wanachama wote mara mbili kwa mwaka.kazi zifuatazo zitafanyika;
a) Kusoma taarifa ya mapato na matumizi ya fedha za shirika
b) Kupitisha bajeti ya shirika
c) Kuidhinisha majina ya wanachama waliopendekezwa kuvuliwa uanachama na kamati kuu kutokana na sababu mbalimbali
(b).Mkutano wa dharula
Wanachama watafanya mkutano wa dharula kulingana naumuhimu na uhitaji wa jambo lenyewe kwa manufaa ya shirika.
20. KUVUNJIKA KWA SHIRIKA
Endapo shirika la YAHFSD litapigiwa kura ya asilimia 99% ya wanachama wote kudai kulivunja shirika.wanachama wote wata takiwa kufanya mambo yafuatayo;
I. kuhakikisha madeni yote ya shirika yanalipwa kwanza kabla ya kuvunjika
II. baada ya malipo yote wanachama wote watagawana gawio la shirila kulingana na aina ya uanachama.
III. Hivyo mwanasheria wa shirika kupitia ofisi ya mkurugenzi ata toa maoni ya kuvunjika kwa shirika na kutiwa saini na mkurugenzi wa shirika.
21. UPITISHAJI WA KATIBA
Katiba hii imepitishwa na kuidhinishwa na wanachama wote waanzilishi wa shirika la YAHFSD katika mutano wao wa hadhara uliofanyika dodoma mjini Tanzania.
22. IMETHIBITISHWA
------------------------------------- --------------------------------------
Geofrey mwakanyamale Jacob,mathias
MWENYEKITI YAHFSD k.n.y. KATIBU MKUU YAHFSD
No comments:
Post a Comment